Mbunge wa Mikumi, Mh. Joseph Haule akiwa na
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi bungeni katika moja ya kikao
cha Bunge kilichopita.
Mbunge wa
jimbo la Mikumi Mh. Joseph Haule amefunguka na kuitaka serikali kuwekeza fedha
za kutosha katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ili wizara hiyo
iweze kuwekeza katika sanaa na kuacha kuwatumia wasanii kama makarai ya
kujengea.
Prof Jay
alisema hayo leo,May 10,2017 Bungeni wakati akichangia makadilio ya mapato na matumizi ya
Wizara ya Habari kwa mwaka 2017 / 2018
"Wasanii
wa Tanzania wamekuwa katika mazingira magumu sana na wamekuwa katika umasikini
mkubwa licha ya mara nyingi kutumiwa katika kampeni mbambali na hata katika
chaguzi zilizopita mmeona jinsi wasanii walivyokuwa wakitumika, mmewatumia kama
makarai na baada ya hapo mmeyaweka uvunguni, tunajua makarai huwa yanatumika
kwenye kujenga maghorofa na vitu vingine lakini nyumba ikikamilika yanawekwa
uvunguni hayatakiwa kuonekana hata kwa wageni" alisema Prof Jay
Mbali na
hilo Prof Jay amesema wasanii wengi wa Tanzania wanakuwa masikini sana sababu
wakishatumika huwa hawathaminiwa tena na kuachwa mpaka wakati mwingine wa
uchaguzi au kampeni
|
No comments:
Post a Comment