Picha Zaidi Baada ya Eneo la Kemondo/Bukoba kuharibika na Magari kupita Barabara ya Katerero/Kyetema. - Mwana Wa Makonda

Breaking

X-BET


Post Top Ad

Saturday, May 13, 2017

Picha Zaidi Baada ya Eneo la Kemondo/Bukoba kuharibika na Magari kupita Barabara ya Katerero/Kyetema.

Mawasiliano yamekuwa ya tabu  kwa Magari na Wasafiri wanaotumia Barabara Kuu inayounganisha Mji wa Bukoba mkoani Kagera na Maeneo jirani ya Mkoa wa Geita, Mwanza na Shinyang’a, kutokana na barabara hiyo kuu kuharibika vibaya eneo la Kemondo kama picha zinavyoelezea.

Barabara hiyo imekatika Jana Ijumaa May 12, 2017 saa 11:00 alfajiri kutokana na mvua iliyonyesha usiku kucha na kusababisha maji kujaa kwenye karavati.
Baada ya Eneo la Kemondo katika barabara ya Bukoba-Muleba kuharibika na magari kuhamia barabara ya Katerero kutokea Kyetema pia magari yameshindwa kupita baada ya gari namba T 913 ASE aina ya Fuso kuharibikia njiani na gari aina ya Benz Semitrail ( Pichani ) kutaka kupita nalo kukwama na kusababisha Msongamano wa magari na abiria .

Hata hivyo tatizo hilo limeisharekebishwa na magari yanaendelea na safari kama kawaida.

Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanroads) Mkoa wa Kagera, Bw.Andrew Kasamwa amesema jitihada zinafanywa kukarabati eneo hilo ili kurejesha mawasiliano.


Post Bottom Ad