Picha -Reli ya kisasa ‘standard gauge’ ilivyozinduliwa rasmi nchini Kenya. - Mwana Wa Makonda

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, May 31, 2017

Picha -Reli ya kisasa ‘standard gauge’ ilivyozinduliwa rasmi nchini Kenya.


Pichani ni Rais Kenyata kwenye uzinduzi wa reli ya kisasa mapema leo mjini Mombasa.

Leo May 31, 2017 ni siku nzuri sana kwa wakenya wanaoishi au wenye ndugu zao kwenye miji ya Mombasa na Nairobi kwani adha ya usafiri wa ardhini haitakuwepo tena baada ya uzinduzi wa reli ya kisasa ya kiwango cha kati (Standard Gauge) ambayo itawapungunguzia adha zote za usafiri ikiwemo muda.

Uzinduzi huo wa reli ya kisasa uliofanyika leo mapema mjini Mombasa na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyata umeigharimu Kenya kiasi cha bilioni 327 za Kenya na unatarajiwa kuchochea sekta ya uchukuzi na usafirishaji kati ya miji hiyo mikubwa ya kibiashara nchini Kenya.

Treni za mizigo zilianza kazi jana na ile ya abiria iliyopewa jina la Madaraka Express imeanza kazi leo kwa kusafirisha abiria kutoka Mombasa hadi Nairobi.


Treni hizo zinazotembea umbali wa kilometa 120 kwa saa zitatumia masaa manne tuu kusafirisha abiria au mizigo kati ya Mombasa na Nairobi.


Kuhusu nauli ya Treni hizo kwa daraja la kawaida tiketi zitauzwa kwa Ksh 900 huku daraja la biashara nauli ikiwa ni Ksh 3000.

Hapa chini Tazama picha za Uzinduzi huo wa Reli hiyo ya kisasa na nyingine zinazoonesha kila kituo kutoka Mombasa hadi nairobi.

Post Bottom Ad