Hatimaye
kivuko kipya cha MV KAZI kimefanyiwa majaribio ya kubeba abiria na magari kwa mara ya kwanza Jijini Dar es Salaam baada
ya kukamilika kwa matengenezo yake.
Majaribio
hayo yalifanyika kulingana na sheria na taratibu za vyombo vya majini ambayo
inavitaka vyombo vyote vya majini kufanyiwa majaribio kabla ya kuanza kazi ili
viweze kupatiwa cheti cha ubora “Seaworthiness Certificate”.
Awali
wataalam kutoka Chuo cha Ubaharia Dar es Salaam (DMI) waliweza kupima ubora na uimara wa kivuko hicho kwa
kutumia utaratibu wa kuweka mawe yenye kilo zinazolingana na uwezo wa kivuko
pamoja na magunia ya mchanga ili kuweza kupima uwezo wa kivuko kulingana na
mahitaji yaliyoainishwa kabla hakijabeba abiria na mizigo.
Zoezi hili
pia lilihusu kufanyika kwa kipimo cha kuhakikisha kuwa kivuko hakilali upande
mmoja yaani “Inclination test” ambapo kilionyesha Kivuko kiko sawa. Taarifa ya
zoezi hili itakuwa sehemu ya vitu vya makabidhiano wakati wa upokeaji wa
Kivuko.
Ujenzi wa MV
KAZI umegharimu Shilingi Bilioni 7.3 za Kitanzania na kina uwezo wa kubeba
abiria 800 magari 22 sawa na jumla ya tani 170.
Kivuko hicho kitakabidhiwa
rasmi hivi karibuni kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kwa ajili ya kuanza
kutoa huduma kati ya Magogoni na Kigamboni Jijini Dar es salaam na kuongeza
idadi ya vivuko katika eneo hilo kufikia vitatu.
|
Tuesday, May 23, 2017
Picha-Majaribio ya Kivuko Kipya cha MV KAZI.
Tags
# MATUKIO
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
MATUKIO
Labels:
MATUKIO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment