Musukuma: Wabunge Wawili ndo Hawakwenda kwa Waganga Wakati wa Uchaguzi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, May 10, 2017

Musukuma: Wabunge Wawili ndo Hawakwenda kwa Waganga Wakati wa Uchaguzi.

Mbunge wa Geita kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Joseph Kasheku Musukuma amezua mvutano bungeni kufuatia kile alichokisema kuwa wabunge wengi ndani ya Bunge la Tanzania wamepita kwa waganga wa kienyeji kipindi cha uchaguzi, na kama kuna ambao hawajapita ni wawili au watatu.

Musukuma aliyasema hayo alipokuwa akichangia hoja ya Wizara ya Habari kuwa wasanii wanatumiwa wakati wa uchaguzi lakini baada ya uchaguzi wanatelekezwa bila msaada wowote.

Kwa karama niliyonayo nikiangalia humu ndani (Bungeni) wakati wa uchaguzi ni wawili au watatu tu hatujapita kwa Waganga.” alisema Joseph Kasheku Musukuma.

Kauli ya Kasheku ilikuwa wakati akitaka kuonyesha kuwa si wasanii pekee wanaotumika na kutelekezwa baada ya uchaguzi, bali hata waganga wanatumika tena baada ya uchaguzi wanasiasa hao hao wanatumia polisi kuwafukuza.

Kufuatia hali hiyo, Kasheku aliuliza swali, kama serikali haoni kuna umuhimu wa kuwajengea japo chuo waganga hawa ili waweze kupatiwa elimu japo kidogo.

Je, Mheshimiwa Spika, serikali haioni umuhimu wa kujenga chuo cha kuwasaidia waganga hawa hata kama ni kwa elimu ndogo?  aliuliza Kasheku.

Wakati mbunge huyo akiuliza swali lake hilo Bungeni, wabunge wengi walisikika wakitaka anyamaze, huku wengine wakitaka awaombe msamaha kwani wanaamini kauli ya kwenda kwa waganga si ya kweli.

Post Bottom Ad