Kampuni ya SportPesa –Rasmi wadhamini Wakuu wa Klabu ya Simba SC. - Mwana Wa Makonda

Breaking

Post Top Ad

Friday, May 12, 2017

Kampuni ya SportPesa –Rasmi wadhamini Wakuu wa Klabu ya Simba SC.

Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya SportPesa Pavel Slavkov pamoja na Rais wa Klabu ya Simba Evance Aveva wakisaini hati ya makubaliano ya mkataba na ukiwa ni mkataba wa udhamini wa kipindi cha miaka mitano wenye thamani ya Bilion 4.9 uliofanyika leo May 12, 2017 katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa. Kulia ni Mkurugenzi wa SportPesa Tanzania Abbas Tarima.

Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya SportPesa Pavel Slavkov akikabidhiana hati ya makubaliano ya mkataba na Rais wa Klabu ya Simba Evance Aveva ukiwa ni mkataba wa udhamini wa kipindi cha miaka mitano wenye thamani ya Bilion 4.9 uliofanyika leo May 12, 2017 katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa.

Kampuni ya SportPesa imeingia mkataba wa miaka mitano wa kuidhamini klabu ya Simba SC ukiwa na thamani ya Bilion 4.9 .

Kampuni hiyo inayojishughulisha na masuala ya michezo ya bahati nasibu nchini Kenya imeweza kuingia nchini Tanzania na kuja kufanya uwekezaji kwa klabu mbalimbali za mpira wa miguu.

Utiaji saini wa makubaliano ya mkataba huo umefanyika jioni hii katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa na kushuhudiwa na wadau mbalimbali wa mpira nchini.

Rais wa Klabu ya Simba SC, Evance Aveva amesema mkataba huu utaweza kuwasaidia katika kuendelea kutoa hamasa kwa timu yao kufanya vizuri zaidi.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa SportPesa nchini Abbas Tarimba amesema kuwa wamefurahi sana kuingia mkataba na Timu ya Simba na mkataba wao utakuwa katika hatua tofauti kulingana na makubaliano waliyoyaingia.

Amesema kwa mwaka wa kwanza Klabu ya Simba SC watapata milioni 880 na katika miaka mitatu inayofuata watapata nyongeza ya asilimia 6  huku mwaka wa mwisho wa mkataba huo klabu hiyo itafaidika kwa kupata bilioni 1.08.

Mbali na hilo Tarimba amesema kuwa klabu ya Simba SC itafaidika kwa kupata fedha mbalimbali kama hamasa iwapo wataweza kupata ubingwa kwa kupewa bonus ya milioni 100 au kushiriki michuano ya kimataifa.

Kabla ya utiaji saini wa mkataba huo Simba SC iliweza kutoka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Stand United magoli yakifungwa na  Juma Luizio yote mawili huku la Stand United likifungwa na Kasim Selembe.

Post Bottom Ad