Chereko za Yanga SC Kuwa Bingwa wa Ligi Kuu- VPL 2016/2017 - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, May 17, 2017

Chereko za Yanga SC Kuwa Bingwa wa Ligi Kuu- VPL 2016/2017

Shabiki wa Yanga SC na Furaha ya Ushindi uwanjani.

Mabingwa Watetezi wa  Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara,Yanga SC hapo Jana May 16, 2017 wakiwa Jijini Dar es Salaam wameifunga Toto Africans  goli 1-0 na kujihakikishia kwa Asilimia kubwa Kuubeba tena Ubingwa wa Ligi hii kwa msimu 2016/2017 ikiwa kwao ni wa 3 Mfululizo baada ya kufikisha pointi 68 na kurejea kwenye nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi kwa tofauti ya pointi tatu.

 Ikiwa Yanga SC watalitwaa taji la ligi msimu huu itakua ni mara yao ya tatu mfululizo kulibeba taju hilo kuanzia msimu wa 2014/2015, 2015/2016 na msimu huu 2016/2017.
Ushindi wa jana wa Yanga SC ulitokana na Krosi murua ya Fulbeki Juma Abdul ya Dakika ya 81 iliyounganishwa kwa Kichwa mithili ya Kombora cha Amissi Tambwe kilichotingisha Nyavu na kuamsha furaha, nderemo na vifijo kwa Mashabiki wa Yanga ndani na nje ya Tanzania.

Ikiwa imebaki mechi moja kabla ya ligi kumalizika, Simba SC inahitaji kushinda mechi yao dhidi ya Mwadui FC kwa idadi kubwa ya magoli halafu Mbao nayo iifunge Yanga SC kwa idadi kubwa ya magoli ili Simba SC itwae taji la VPL kitu ambacho ni kigumu kulingana na hali ilivyo kwa sasa.


Ratiba/Matokeo:

MECHI ZA MWISHO

Jumamosi May 20,2017.

Azam FC v Kagera Sugar

Maji Maji FC v Mbeya City

Simba  SC v Mwadui FC

Mbao FC v Yanga SC

Stand United v Ruvu Shooting

Mtibwa Sugar v Toto Africans

Tanzania Prisons v African Lyon

Ndanda FC v JKT Ruvu

Post Bottom Ad