Chelsea Yajihakikishia Ubingwa wa EPL 2016/2017 kwa Kuitandika Watford 4-3. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, May 16, 2017

Chelsea Yajihakikishia Ubingwa wa EPL 2016/2017 kwa Kuitandika Watford 4-3.

Antonio Conte.

Kocha wa Chelsea Antonio Conte hili ni kombe lake la 4 ndani ya misimu minne, kabla hajaja Chelsea alichukua makombe matatu ndani ya misimu mitatu iliyopita akiwa na Timu ya Juventus na huu ni wanne kwake na amebeba kombe.


Wachezaji wa Chelsea wakimrusha juu koch wao, Antonio Conte kwa furaha baada ya kujihakikishia Ubingwa wa Ligi Kuu ya England Msimu huu wa 2016/2017 kufuatia ushindi wa 4-3 dhidi ya Watford usiku wa Jumatatu May 15,2017 Uwanja wa Stamford Bridge. 

Mabao ya Chelsea yalifungwa na John Terry dakika ya 22, Cesar Azpilicueta dakika ya 36, Michy Batshuayi dakika ya 49 na Cesc Fabregas dakika ya 88 wakati ya Watford yamefungwa na Etienne Capoue dakika ya 24, Daryl Janmaat dakika ya 51 na Stefano Okaka dakika ya 74. 

Chelsea imefikisha pointi 90 baada ya kucheza mechi 37 na sasa rasmi ni mabingwa wapya, wakirithi taji lililoachwa wazi na Leicester City waliolibeba msimu wa 2015/2016.

John Terry aweka rekodi.

Pamoja na beki huyo kutokuwa na nafasi katika klabu ya Chelsea msimu huu lakini amekuwa kapteni wa kwanza katika historia ya ligi kuu Uingereza kubeba makombe mengi akiwa na matano, anayemfuatia ni Roy Keane mwenye manne.
Ubingwa huo wa Chelsea umeifanya klabu hiyo kuwa na makombe 5 sawa na Manchester United na kuzifanya timu hizo kuongoza kwa idadi ya makombe ya EPL tangu msimu wa mwaka 2003/2004.

Post Bottom Ad