Breaking News: IGP Sirro Awatumia Salam Wanaotekeleza Mauaji na Uhalifu Mwingine nchini Tanzania. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, May 31, 2017

Breaking News: IGP Sirro Awatumia Salam Wanaotekeleza Mauaji na Uhalifu Mwingine nchini Tanzania.Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro kwa mara ya kwanza amefanya mazungumzo maalum na wanahabari Leo May 31,2017 jijini Dar es Salaam ikiwa ni siku mbili tangu Amri Jeshi Mkuu wa nchi, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amuapishe kuwa IGP.

 Katika mazungumzo yake, IGP Sirro amesema suala la mauaji kwa viongozi wa Serikali za Mitaa yanayofanywa na wahalifu wilayani Rufiji, Kibiti, Ikwiriri na Mkuranga Mkoa wa Pwani ni jambo la muda mfupi ambalo hivi karibuni majibu sahihi yatapatikana.

“Wanahabari niseme tu kwamba nchi yetu ni shwari, hatuna matukio makubwa ya kutisha, lakini changamoto kubwa ni Mkoa wa Pwani ambako baadhi ya raia wema wameuawa bila sababu, kuna kikundi cha watu wachache wanaodhani wanaweza kuufanya ule mkoa kukosa amani. Lakini haki lazima itatoa majibu.

“Niwahakikishie Watanzaia kwamba suala la Ikwiriri, Mkuranga na Rufiji ni la muda mfupi, viongozi wangu wamezungumza ukianza na Rais (Dkt. John Pombe Magufuli), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi (Mwigulu Nchemba) hivyo mimi sina la kuzungumza zaidi ya kufanya kazi kwa weredi.
“Aidha Sirro amesema Jeshi la Polisi linapeleka salam kuwa ubaya wanaoufanya na wahalifu huko Pwani, wataujibu kwa ubaya kwa mujibu wa sheria. Amesema IGP SIrro.

Kuhusu wanaotumia bodaboda kufanya uhalifu, amesema hakuna mtu alie juu ya sheria. Amesema bodaboda wanapita kwenye taa nyekundu, wanapita wakiwa kwenye mshikaki. Amewapa salam kuwa ni wakati wa utii wa sheria.

Sirro amewaonya watu wanaojihusisha na madawa ya kulevya.

Watu wenye hasira kali nao wameguswa akitolea mfano wezi wa kuku na kuhoji kama kuku ana thamani sawa na mhusika. Amesisitiza kama amekosa akamatwe na apelekwe mahakamani na kusema anayejifanya ana hasira kali itamfanya aiache familia yake.

Kuhusu askari kujihusisha na rushwa, amesema hakuna askari atakaejihusisha na Rushwa na akabaki salama na kusema ameshatoa maelekezo kwa jeshi polisi kuwa atakaefanikisha kupatikana kwa wala rushwa atapata zawadi.


Sirro pia ameahidi kutoa shilingi milioni 10 kwa raia mwema atakayetoa taarifa sahihi kwa watu wanaotekeleza mauaji Kibiti, Mkuranga, Rufiji na Ikwiriri Pwani. BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUMSIKILIZA IGP Sirro AKIZUNGUMZA
  

Post Bottom Ad