VPL-2016/2017: Yanga SC Yarejea kileleni kwa Muda ikiifunga Azam FC 1-0. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, April 01, 2017

VPL-2016/2017: Yanga SC Yarejea kileleni kwa Muda ikiifunga Azam FC 1-0.

Mabingwa watetezi wa Ligi kuu ,Yanga SC wamerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2016/2017 baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC jioni ya leo April 1, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Goli la Yanga SC limefungwa na mfungaji Mzambia Obrey Chirwa dakika ya 70 baada ya kumtoka beki wa Azam FC, Mghana Yakubu Mohamed kufuatia pasi ndefu ya kiungo Mnyarwanda, Haruna Niyonzima.

Ushindi huo unaifanya Yanga SC sasa ifikishe pointi 56 baada ya kucheza mechi 25 na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu kwa muda ikiwaangushia nafasi ya pili mahasimu wao, Simba SC wenye pointi 55 ambao kesho April 02, 2017 watacheza mechi ya 25 pia dhidi ya Kagera Sugar mjini Bukoba.

Post Bottom Ad