VPL-2016/2017-Msimamo wa Ligi Ulivyo sasa baada ya Kagera Sugar kumfunga Simba SC bao 2-1 -Kaitaba/Bukoba. - Mwana Wa Makonda

Breaking

Post Top Ad

Sunday, April 02, 2017

VPL-2016/2017-Msimamo wa Ligi Ulivyo sasa baada ya Kagera Sugar kumfunga Simba SC bao 2-1 -Kaitaba/Bukoba.

Simba SC wakiingia Uwanja wa Kaitaba-Bukoba.

Timu ya Kagera Sugar wameipunguza kasi Simba SC katika mbio za ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara hii leo April 2, 2017 baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera.
Kipigo walichopata Simba kinawarudisha chini hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara wakibaki na pointi zao 55 na Yanga sasa inaongoza ligi kwa tofauti ya pointi moja huku timu zote zikiwa zimeshacheza mechi 25.

Kagera Sugar ndio walitangulia kufunga Dakika ya 27 kwa mzinga mkali wa Mbaraka Yusuf na Bao hilo kudumu hadi Haftaimu.

Kipindi cha Pili Dakika 47, Kagera Sugar walienda 2-0 mbele kwa Bao la Edward Christopher.
Simba SC walipata Bao lao pekee Dakika ya 67 kupitia Muzamil Yassin.

Jumapili Aprili 02,2017.

Kagera Sugar 2 – 1 Simba SC

African Lyon 1 – 0 Stand United 

Tanzania Prisons 0 – 0 Mtibwa Sugar 

Mwadui FC 2 – 2 JKT Ruvu 

Maji Maji FC 4 – 1 Toto Africans

MSIMAMO WA LIGI ULIVYO SASA.

Post Bottom Ad