Tazama Wabunge walivyomshangilia Rais Mstaafu JK – Bungeni Dodoma. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, April 04, 2017

Tazama Wabunge walivyomshangilia Rais Mstaafu JK – Bungeni Dodoma.

Mkutano wa Saba wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umeanza leo,April 04,2017 Mjini Dodoma. Mkutano huu ni kwa ajili kupitisha Bajeti ya Serikali 2017/2018 itakayowasilishwa Bungeni June 15 mwaka huu.

Pia Wabunge wa Bunge la Jmahuri ya Muungano wa Tanzania leo Aprili 4, 2017 wameonyesha upendo wao wa dhati ‘mahaba’ kwa Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipoibuka Bungeni Kushuhudia kuapishwa kwa mkewe, Mama Salma Kikwete aliyeteuliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli hivi karibuni kuwa Mbunge.

Wabunge hao hawakutaka kuficha hisia zao kuonesha kuwa wamemmiss Mzee Kikwete walianza kumshangilia kwa nguvu mara baada ya Spika Job Ndugai kutambulisha ugeni wake, huku wengine wakichombeza kuwa wamemkumbuka Kikwete na wangetamani ashuke kutoka viti vya juu (ambako huketi wageni) ili akasalimiane na Spika.
Akiwa bungeni, Rais Kikwete alisaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Mbunge wa Viti Maalum-CHADEMA, marehemu Dkt. Elly Macha.

HAPA CHINI TAZAMA VIDEO NAMNA WABUNGE WALIVYOMSHANGILIA JK

Post Bottom Ad