Taswira Picha ya Shule mpya ya msingi Rubondo wilayani Biharamulo Mkoani Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, April 22, 2017

Taswira Picha ya Shule mpya ya msingi Rubondo wilayani Biharamulo Mkoani Kagera.

Shule mpya ya msingi Rubondo iliyoko Kitongoji cha Nyarukongogo Mamlaka ya mji mdogo wa Biharamulo Mkoani Kagera.

Mwenyekiti wa  Halmashauri ya wilaya ya Biharamulo,Mhe. Afsa Galiatano na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Bi.Wende Ng'ahala wakikagua ujenzi wa madarasa manane na  matundu 20 ya vyoo  ya shule mpya ya msingi Rubondo iliyoko Kitongoji cha Nyarukongogo Mamlaka ya mji mdogo wa Biharamulo Mkoani Kagera.

Walikagua madarasa hayo manane na vyoo vya wanafunzi 900 watakaohamia katika madarasa hayo mapya baada ya kuboresha ya awali ambayo walisoma kwa msongamano wa wanafunzi 80 darasa moja na sasa watakuwa ni wanafunzi 45 ambapo ujenzi umegharimu Sh 190 Milioni.
Pia shule hiyo imewekewa miundombinu ya maji na umeme na madawati 240 yenye thamani ya Sh12mil na imejengwa kwa kutumia wakandarasi, mafundi na vibarua wa kawaida  wakiwa ni wazaliwa wa kitongoji hicho ambacho awali kilikuwa ni kijiji kabla ya kuwa ndani ya Mamlaka ya Mji wa Biharamulo
Mwenyekiti huyo wa Halmashauri na Mkurugenzi walikagua ujenzi wa madarasa hayo jana na kushauri Mwenyekiti wa kamati ya shule Mathias kagimba kuharakisha ukamilishaji wa miundombinu ili wanafunzi wahamie kwenye madarasa hayo ifikapo Julai mwaka huu.

Habari/Picha Na-Shaban Nasib Ndyamukama.

Post Bottom Ad