Taswira Picha Ukaguzi wa Eneo la Parking Bay Benaco/Ngara-Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, April 25, 2017

Taswira Picha Ukaguzi wa Eneo la Parking Bay Benaco/Ngara-Kagera.

Wajumbe wa kamati fedha, utawala na mipango pamoja na wataalam wakikagua mradi wa parking bay Benaco katika kata Kasulo kijiji cha Rwakalemera. Mradi huo unagharimu kiasi cha shilingi milioni 148 ikiwemo na VAT ndani yake na mkandarasi anayeshughulikia mradi ni ACIA Company Limited. 

Mradi ulianza tarehe 03/03/2017 na unatarajia kumalizika tarehe 30/6/2017 na unagharamiwa na fedha za mfuko wa miradi ya maendeleo. 

Wajumbe waliridhishwa na jinsi mradi unavyoendelea na kumsihi mkandarasi kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati ili kuendana na usemi wa sasa wa serikali ya awamu ya tano wa hapa kazi tuu.
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ngara Aidan Bhama (mwenye nguo nyeusi) akijadiliana na waheshimiwa madiwani kuhusiana na ujenzi wa parking bay na namna mapato ya halmashauri yatakavyoongezeka pindi mradi huo utakapokamilika.

Post Bottom Ad