Taswira Picha hali ilivyo Benaco kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha na Staili ya Kuegesha Magari kandokando ya Barabara Kuu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, April 10, 2017

Taswira Picha hali ilivyo Benaco kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha na Staili ya Kuegesha Magari kandokando ya Barabara Kuu.

Barabara ya Benaco-Rusumo na hapa ni eneo la Benaco,Kata ya Kasulo wilayani Ngara mkoani Kagera,mambo yalikuwa namna hii,wenye magari makubwa walipita kwa staili ya tahadhali baada ya mvua kunyesha na eneo hilo kujaa matope mazito na yenye utelezi sambamba na madimbwi ya maji kandokando ya barabara hiyo na kupelekea adha kubwa kwa wakazi wa eneo hilo ambalo kwa muda sasa huwa linajaa magari njia nzima likitumika kama eneo la kuegesha au kupaki magari makubwa ya mizigo yatokayo na kwenda nchi Jirani ya Rwanda.


Magari makubwa na Madogo yakiwa yamepaki kusubiri taratibu mbalimbali za kuvuka boda ya Rusumo ambao ni mpaka baina ya Tanzania na Rwanda ama wahusika wake kupata huduma mbalimbali za Kijamii katika eneo la Benaco,kata ya Kasulo wilayani Ngara mkoani Kagera ,huku taswira ikionekana ya eneo hilo kukosa namna bora ya kubuniwa ili kuwa chanzo cha mapato hasa kwa wanaolitumia kuegesha magari yao kando ya barabara hiyo kwani hakuna utaratibu mzuri na wakati mwingine huatarisha usalama wa matumizi sahihi ya barabara hiyo kuu ya kutoka Lusahunga-Benaco-Rusumo.

Post Bottom Ad