Ifahamu Ratiba ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). - Mwana Wa Makonda

Breaking

X-BET


Post Top Ad

Sunday, April 23, 2017

Ifahamu Ratiba ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).


Yanga SC itamenyana na Mbao FC katika Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), au Azam Sports Federation Cup (ASFC), Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, lakini Nusu Fainali kali zaidi inatarajiwa kuwa kati ya Azam FC na Simba SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Nusu Fainali ya kwanza itapigwa Aprili 29,2017 Uwanja wa Taifa Jijini na ya pili Aprili 30,2017 Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Hiyo inafuatia droo iliyopangwa leo,April 23, 2017 studio za Azam TV, wadhamini wa michuano hiyo, Tabata mjini Dar es Salaam.

Ikumbukwe Yanga SC jana ilikamilisha idadi ya timu za Nusu Fainali za mwaka huu kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tanzania Prisons ya Mbeya Uwanja wa Taifa.

Post Bottom Ad