Ratiba ya Mechi za Ligi kuu VPL 2016/2017 – Wiki endi hii Toto na Simba SC. - Mwana Wa Makonda

Breaking

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, April 12, 2017

Ratiba ya Mechi za Ligi kuu VPL 2016/2017 – Wiki endi hii Toto na Simba SC.

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea kuanzia Kesho Alhamisi April 13, 2017 kwa timu ya Mbeya City itaikaribisha African Lyon ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya katika mchezo utakaoanza saa 10.00 jioni.

 Jumamosi ya Aprili 15, mwaka huu,2017 kutakuwa na michezo minne ambako Stand United itakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga wakati Toto Africans ya Mwanza itaialika Simba SC ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Mechi hizi, zitachezwa kuanzia saa 10.00 jioni.

Kadhalika siku hiyo ya Jumamosi, Majimaji FC ya Songea itakuwa mgeni wa Ruvu Shooting ya Pwani kwenye Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani - mchezo utakaoanza saa 8.00 mchana ilihali JKT Ruvu ikiwa kwenye Uwanja wake mpya wa nyumbani - Mkwakwani jijini Tanga itaialika Azam FC ya Dar es Salaam kuanzia saa 10.00 jioni.

Kwa mujibu wa ratiba, Jumapili Aprili 6, mwaka huu,2017  Mbao FC itacheza na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza huku Mwadui FC ikiwa mwenyeji wa Ndanda FC ya Mtwara kwenye Uwanja wa Mwadui mkoani Shinyanga. Kadhalika, mechi hizo zitaanza saa 10.00 jioni.

IMETOLEWA NA TFF

Post Bottom Ad