Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiwa katika Gari
maalum na kuwapungia mkono Wananchi mbali mbali wa Mji wa Dodoma wakati wa
sherehe za miaka 53 ya Muungano wa Tanzania zilizofanyika leo April 26, 2017 katika Uwanja wa Jamhuri.
|
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais
Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwenye sherehe za Miaka 53
ya Muungano katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe
26 April 2017, ameongoza maelfu ya Watanzania katika sherehe za miaka 53 ya
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mjini
Dodoma.
Akizungumza
mara baada ya kukagua gwaride la vikosi vya ulinzi na Usalama lililoandaliwa
kwa heshma yake, Rais Magufuli amewahakikishia watanzania kuwa yeye na Rais wa
Zanzibara Dkt. Ali Mohamed Shein wataendelea kuulinda Muungano kwa nguvu zao
zote na kwamba atakayejaribu kuuvunja atavunjika yeye.
''Muungano
ndio silaha yetu. Ni nguvu yetu. Mimi na mwenzangu Dkt. Shein tutaulinda
Muungano kwa nguvu zote. Yeyote
atakayejaribu kuuvunja atavunjika yeye'' amesema Rais Magufuli.
Aidha Dkt.
Magufuli amewataka watanzania kuendelea kudumisha amani iliyopo nchini kwani
amani ndio chachu ya maendeleo yanayopatikana nchini.
Rais
Magufuli amesema Tanzania imeweza kufikisha miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika
na Zanzibar kwa sababu ya amani iliyopo nchini iliyowezesha kupatikana
mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuunganisha mataifa yetu mawili na kuuunda
taifa moja lenye nguvu.
Aidha
amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar umewezesha kupatikana mafanikio
makubwa katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii.
Mhe. Rais
ametaja mafanikio mengine yaliyopatikana kutokana na Muungano ni kukua kwa
uchumi na kukabiliana na matatizo ya umasikini na ukosefu wa ajira,kuimarisha
miundombinu ya usafiri wa anga, majini,reli
na nchi kavu.
Aidha
Muungano umeimarisha na kuboresha upatikanaji wa huduma za jamii ikiwa ni
pamoja na kuongezeka kwa idadi ya shule na hospitali pamoja na kukua kwa
demokrasia nchini.
Kwa mara ya
kwanaza katika historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Maadhimisho ya
Sherehe za Muungano zinafanyika mkoani Dodoma makao makuu ya Serikali ikiwa ni
ishara tosha kuwa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na chama cha Mapinduzi
imedhamiria kwa dhati kuhakikisha makao makuuu ya Serikali yanakuwa Dodoma.
''Niwahahakikishie
wana Dodoma na Watanzania kwa ujumla
kwamba Serikali sasa tumefika Dodoma na hatutarudi tena, na kama tulivyoahidi mwaka 2020 Serikali yote
itakuwa imehamia hapa'' amesema Rais magufuli.
Sherehe za
miaka 53 ya Muungano zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na
wajane wa viongozi waasisi wa Muungano mke wa hayati Mwalimu Julius Nyere Mama
Maria Nyerere na hayati Abeid Aman Karume, Mama Shadya Karume,Makamu wa Rais
Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, na viongozi wa chama na
serikali.
Kauli mbiu
ya Sherehe za Muungano mwaka huu ni ''Miaka 53 ya muungano,Tuuulinde na
kuuimarisha, Tupige vita Dawa za Kulevya na Kufanya Kazi kwa Bidii''
Jaffar Haniu
Naibu
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dodoma
26 Aprili,
2017
|
No comments:
Post a Comment