Picha:Licha ya Sare ya 2-2,Mashabiki kwa mara nyingine washinikiza Meneja Arsene Wenger ang’oke, Arsenal. - Mwana Wa Makonda

Breaking

X-BET


Post Top Ad

Sunday, April 02, 2017

Picha:Licha ya Sare ya 2-2,Mashabiki kwa mara nyingine washinikiza Meneja Arsene Wenger ang’oke, Arsenal.

Meneja wa Arsenal -Arsene Wenger ndani ya taswira nzito.

Ndani ya dimba la nyumbani la  Emirates ambako baadhi ya Mashabiki kwa mara nyingine walileta shinikizo ili Meneja Arsene Wenger  ang’oke, Arsenal wanatoka  nyuma na kuambulia Sare ya magoli 2-2  dhidi ya Manchester City na kubakia Nafasi ya 6 kwenye Msimamo wa Ligi Kuu England 2016/2017 jioni ya Leo April 2, 2017.  


Beki wa kati wa Arsenal, Shkodran Mustafi akikimbia kushangilia baada ya kuifungia timu yake bao la kusawazisha dakika ya 53 ikitoa sare ya 2-2 na Manchester City katika mchezo wa Ligi Kuu.
Bao lingine la Arsenal lilifungwa na Theo Walcott dakika ya 40, wakati ya Man City yamefungwa na Leroy Sane dakika ya tano na Sergio Aguero dakika ya 42.

EPL itarindima tena Jumanne na Jumatano kwa Timu zote 20 kuwa dimbani na Bigi Mechi, bila shaka, ipo Jumatano Stamford Bridge wakati Vinara Chelsea wakiivaa Man City.

Post Bottom Ad