Picha/Habari-Watu 27 Wafariki ajalini Eneo la Mtito Andei, Kenya. - Mwana Wa Makonda

Breaking

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, April 25, 2017

Picha/Habari-Watu 27 Wafariki ajalini Eneo la Mtito Andei, Kenya.

Muonekano wa basi baada ya kupata ajali na watu 27 wamefariki leo April 25, 2017 na wengine kujeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kugongana na lori huko Kambu, Mombasa nchini Kenya.

Ajali hiyo imelihusisha basi la kubeba abiria na lori la kusafirisha mafuta ghafi ya kupikia ilitokea katika eneo la Kambu, karibu na Mtito Andei.

Awali Mkuu wa polisi wa eneo la Kibwezi Leonard Kimaiyo ameviambia vyombo vya habari kuwa watu 23 walifariki papo hapo na Watu 20 walipata majeraha na kupelekwa katika hospitali za miji ya Kibwezi na Makindu.
 Basi likiwa katika muonekano mbaya baada ya kupata ajali.
Muonekano wa Lori baada ya kupata ajali.

Bw Kimaiyo amesema walionusurika waliambia maafisa wa polisi dereva wa basi alikuwa akijaribu kupita gari jingine basi lilipogongana na lori hilo.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Taifa ya Uchukuzi Kenya, watu 3,000 hufariki kila mwaka kutokana an ajali za barabarani.
 

Post Bottom Ad