Picha/Habari –China na Uzinduzi wa Meli kubwa ya Kubeba Ndege za kivita. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, April 26, 2017

Picha/Habari –China na Uzinduzi wa Meli kubwa ya Kubeba Ndege za kivita.

Meli ya kwanza ya kubeba ndege ya China kwa Liaoning ilinunuliwa kutoka Ukraine.

China imetangaza kwamba imefanikiwa kuzindua manowari yake ya kwanza ya kujiundia yenye uwezo wa kubeba ndege za kivita.

 Meli hiyo ya kivita ina uzani wa tani 50,000.

Hatua hiyo inachukuliwa kama ishara ya karibuni zaidi ya kujiimarisha kwa taifa hilo katika nguvu za jeshi lake la majini.

Vyombo vya habari nchini China vinasema meli hiyo, ambayo inawezesha ndege kuruka na kutua juu yake, ilisafirishwa kutoka eneo ambalo ilikuwa ikiundiwa Dalian na kuwekwa baharini.

Inatarajiwa kuanza kazi rasmi mwaka 2020.

Meli ya Liaoning ilipokuwa inakabidhiwa rasmi kwa jeshi la wanamaji la China Septemba 2012.

Meli pekee kubwa ya kubeba ndege inayomilikiwa na China ni meli ya Liaonong, ambayo ni meli ya enzi za muungano wa Usovieti iliyofanyiwa ukarabati.

China ilinunua meli hiyo kutoka kwa Ukraine.
Meli hiyo baada ya kung'oa nanga Dalian.

Meli hiyo ya kivita ilizinduliwa Dalian.


Vyombo vya habari vya serikali ya China vimesambaza picha za manowari hiyo ikiwa imerembeshwa kwa mapambo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad