Nusu Fainali ya FA CUP-Chelsea yamsubiri Fainali kati ya Arsenal au Manchester City. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, April 22, 2017

Nusu Fainali ya FA CUP-Chelsea yamsubiri Fainali kati ya Arsenal au Manchester City.

Wachezaji wa Chelsea wakishangilia kwa furaha baada ya timu yao kuibuka mshindi wa bao 4-2 dhidi ya Tottenham Hotspur  katika mchezo wa Nusu Fainali ya FA CUP  iliyochezwa leo April 22, 2017 huko London Uwanja wa Wembley.

 


Eden Hazard akiteleza chini kushangilia baada ya kuifungia bao la tatu Chelsea dakika ya 75 katika ushindi wa 4-2 dhidi ya Tottenham Hotspur leo Uwanja wa Wembley katika Nusu Fainali ya Kombe la FA England. 

Willian amefunga mabao mawili moja dakika ya tano na lingine dakika ya 43 kwa penalti wakati bao lingine la Chelsea limefungwa na Nemanja Matic dakika ya 80 huku ya Spurs yakifungwa na Harry Kane dakika ya 18 na Dele Alli dakika ya 52. 


Chelsea sasa itakutana na mshindi kati ya Arsenal au Manchester City zinazomenyana kesho April 23, 2017 Wembley

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad