Nusu Fainali Ulaya 2016/2017-Bingwa Mtetezi na Atletico Madrid huku Juventus na Manaco. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, April 21, 2017

Nusu Fainali Ulaya 2016/2017-Bingwa Mtetezi na Atletico Madrid huku Juventus na Manaco.

Jiji la Madrid ,Hispania litashuhudia Wapinzani katika Soka  Real Madrid na Atletico Madrid wakikutana katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu wa 2016/2017.

Nusu fainali nyingine itakuwa kati ya Juventus ya Italia na Monaco ya Ufaransa.
Katika marudio ya fainali ya msimu uliopita 2015/2016, mahasimu hao wa La Liga watakutana Uwanja wa Bernabeu Mei 2,2017 na mchezo wa marudiano utafanyika Uwanja wa Vicente Calderon.

Monaco watakuwa wenyeji wa mabingwa wa Serie A, Juventus Uwanja wa Louis II Mei 3,2017 kabla ya kusafiri kwenda Turin kwa mchezo wa marudiano Mei 10,2017. 

Uwanja wa Cardiff ndiyo utakaohodhi fainali ya michuano hiyo Juni 3,2017 hiyo ikiwa mara ya kwanza mfalme wa Ligi ya Mabingwa anapatikana katika ardhi ya Wales.

Post Bottom Ad