Kuhusu suala
la Ngono kua chanzo kikubwa cha UTI, ni dhana inayotokana na imani iliyojengeka
kwa baadhi ya watu kwneye jamii.
Dr Isaac
Maro amefafanua hayo kwa kupitia akaunti yake ya Instagram kwa maelezo
yafuatayo.
1) Kwanza,
inasemekana kwamba UTI inaambukiza – yaani kwamba unaweza kumwambukiza mwenzi
wako. Tukizungumza kiujumla, UTI (maambukizi kwenye mfumo wa mkojo)
hayaambukizi, hapa tunamaanisha huwezi kupata UTI kutoka kwa mwenza wako kama
ungefanya naye mapenzi/ngono.
ILA , kama UTI ya huyo mwenza wako ilisababishwa
na ugonjwa wa ngono ( maana kuna UTI zinazosababishwa na magonjwa ya ngono kama
chymadia au trichomoniasis – hii hutokea pale bacteria wanaposambaa kwenye
urethra ) basi wewe utakuwa hatarini kupata hayo magonjwa ya ngono hadi pale
mwenzi wako atakapotibiwa.
Hivyo basi, kitendo cha ngono chenyewe hakiwezi moja
kwa moja kusababisha UTI bali kinaweza kuchangia katika kusukuma bacteria
(vimelea) kwenye mrija wa mkojo) na kusababisha muwasho katika hili eneo na
hili linaweza kuongeza uwezekano wa mtu kupata UTI.
2) Pili,
inasemekana kwamba watu wanaofanya ngono ndio hao tu wanaopata maambukizi haya.
Hapana, UTI inaweza kutokea wakati wowote maishani, hata kama mtu hajaanza
kujamiiana – ingawa UTI inawatokea sana wanawake wajawazito, na watu wazima.
Kujamiiana kunaweza kuamsha maambukizi ya mfumo wa mkojo lakini haumweki mtu
kwenye hali ya hatari kupata maambukizi haya.
3) Tatu,
kwenda haja ndogo baada ya ngono kunakinga maambukizi ya UTI.
Hii ni kweli pale
mtu anapokojoa haswa mpaka kibofu kinakuwa kitupu bila mkojo.
|
Wednesday, April 26, 2017
Ngono Isihusishwe na Mkojo Mchafu -UTI.
Tags
# DONDOO
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
DONDOO
Labels:
DONDOO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment