Mbunge Freeman Mbowe,Halima Mdee,RC Makonda na DC Mnyeti Kufika Kamati ya Maadili ya Bunge Kujieleza. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, April 06, 2017

Mbunge Freeman Mbowe,Halima Mdee,RC Makonda na DC Mnyeti Kufika Kamati ya Maadili ya Bunge Kujieleza.

Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ameliagiza Jeshi la Polisi kumkamata na kumfikisha Bungeni Mbunge wa Kawe (CHADEMA) Halima Mdee kwa tuhuma za kutumia lugha za matusi.

Spika Ndugai ameagiza mbunge huyo kukamatwa akiwa bungeni mjini Dodoma.

Kwahiyo Halima Mdee popote alipo katika nchi hii, najua hayupo Dodoma by saa hii awe yeye mwenyewe awe amejileta bungeni. La sivyo akamatwe na polisi popote pale alipo aletwe kwa pingu hapa bungeni hatuwezi kucheza katika mambo ya msingi, tuelewane kabisa tumekuja mmoja mmoja hapa,” amesema Spika Ndugai

Mbunge huyo alitoa lugha za matusi kwa Spika wakati wa uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki uliofanyika April 4, 2017.
Pia Mbunge Freeman Mbowe ameagizwa na Spika Ndugai kufika mbele ya Kamati ya Maadili leo akituhumiwa kutukana Bunge kufuatia uchaguzi huo  wa EALA.

Mwingine anayetarajiwa kuhojiwa na Kamati ya Bunge ya Kinga, Maadili na Madaraka leo ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Pastory Mnyeti ambaye ameitwa na kamati hiyo  na anatakiwa kufika leo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad