Matukio Picha-Kagera Sugar walivyoshangilia kuifunga Simba SC-Kaitaba. - Mwana Wa Makonda

Breaking

X-BET


Post Top Ad

Sunday, April 02, 2017

Matukio Picha-Kagera Sugar walivyoshangilia kuifunga Simba SC-Kaitaba.

Wachezaji wa Timu ya Kagera Suger wakifurahi kwa pamoja na Kocha wao Mecky Mexime baada ya mchezo kumalizika leo April 2, 2017 uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba na Kufanikiwa kuifunga Simba SC bao 2-1.

Katika mchezo huo wa Ligi kuu,Simba SC sasa inakubali kipigo cha nne cha VPL dhidi ya  Kagera Sugar na Kagera Sugar kufikisha pointi 45 baada ya michezo 25.

Juma Kaseja akipokea zawadi ya fedha kutoka kwa moja ya Shabiki wa Timu ya Kagera Sugar kufuatia kuwa ngome kubwa ya kuizuia Simba SC isipate ushindi katika  mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Kaitaba.

Kaseja alipangwa langoni dhidi ya timu aliyopata nayo mafanikio tangu mwaka 2003 hadi 2009 alipohamia Yanga SC kabla ya kurejea 2011 na kudaka tena hadi 2013 alipohamia Yanga SC alikocheza kwa misimu miwili kabla ya kuhamia Mbeya Ciy na sasa yuko Kagera Sugar anamalizia soka yake.Post Bottom Ad