Matokeo ya FA Cup - Yanga SC yaungana Nusu Fainali na Simba SC,Mbao FC na Azam FC.Prisons April 22, 2017 - Mwana Wa Makonda

Breaking

Post Top Ad

Saturday, April 22, 2017

Matokeo ya FA Cup - Yanga SC yaungana Nusu Fainali na Simba SC,Mbao FC na Azam FC.Prisons April 22, 2017

Amissi Tambwe akiifungia kwa kichwa Yanga leo Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mabingwa wa tetezi wa kombe la shirikisho (FA) Yanga SC, wametinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tanzania Prisons.

 Yanga SC ilipata magoli yake kupitia kwa Amissi Tambwe aliyefunga dakika ya 16 ya mchezo, Obrey Chirwa akafunga bao la pili dakika ya 41 na kuifanya Yanga SC kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-0.
Mchezo huo wa robo fainali umefanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambapo Yanga SC sasa inaungana na mahasimu wao Simba SC, Azam FC na Mbao FC katika hatua inayofuata ambayo ni nusu fainali.

Droo ya Nusu Fainali inatarajiwa kuchezeshwa kesho April 23, 2017 Saa 11:00 jioni katika studio za Azam TV, wadhamini wa michuano hiyo, zilizopo Tabata mjini Dar es Salaam.

Post Bottom Ad