Marehemu Mh. Elly Macha aagwa Rasmi - Mwana Wa Makonda

Breaking

X-BET


Post Top Ad

Friday, April 21, 2017

Marehemu Mh. Elly Macha aagwa Rasmi

Waziri mkuu Mh. Kassim Majaliwa pamoja na wabunge mbalimbali wameshiriki kuuaga mwili wa aliyekua mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Dkt Elly Macha, aliyefariki nchini Uingereza alipokuwa akipatiwa matibabu.

Mwili huo umewasili alfajiri leo,April 21,2017 katika uwanja wa Mwalimu Nyerere ambapo mapokezi yaliongozwa na Naibu spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Tulia Ackson na kusafirishwa tena mpaka Dodoma ambapo viongozi wa bunge wamepata fursa ya kuuaga Mheshimiwa Macha kwenye viwanja hivyo vya bunge.

Dkt Macha alifariki dunia Machi 31 mwaka huu katika hospitali ya New Cross, Wolverhampton iliyopo nchini Uingereza alipokuwa akipatiwa matibabu.

Aidha Naibu spika, Dk Tulia Ackson amesema Bunge lilipata taarifa za ugonjwa wa marehemu ndani ya miezi mitatu na baadae kupata taarifa juu ya kifo chake na kusema kwamba, licha ya kua na ulemavu, Dkt Macha alipigania haki za walemavu kijasiri na kikamilifu.

Post Bottom Ad