Kabila la Wala Watu- Wanawake Hujifunga Magome ya Miti au Majani Maalum Kuanzia Kiunoni na Matiti Huachwa Wazi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, April 18, 2017

Kabila la Wala Watu- Wanawake Hujifunga Magome ya Miti au Majani Maalum Kuanzia Kiunoni na Matiti Huachwa Wazi.

mwanajamii wa kabila la wala watu wakifanya jambo la kimila.

Wiki iliyopita nilieleza jinsi wanawake wa taifa hilo ambalo jamii yake inakula nyama za watu kutokana na mila potofu.

Serikali ya Visiwa vya Papua New Guinea vimekuwa vikilaumiwa kutokana na kutowatetea wanawake wa nchi hiyo licha ya kupewa mateso mbalimbali na wanaume au waume zao.

Serikali hiyo inalaumiwa kutokana na kutunga sheria mwaka 1971 ambayo inahusiana na mambo ya uchawi.

Sheria hiyo inalaumiwa kwa sababu inawalenga wanawake kitu ambacho kinawashangaza wengi hasa wanawake wa huko hasa wale waliobahatika kupata elimu.

Mwaka 2013 serikali ya nchi hiyo ilitunga sheria ya kupiga marufuku kuwapiga wanawake majumbani bila shaka baada ya kuona wanawake wengi wakipigwa, kudhalilishwa na wengine kufa au kupewa vilema vya maisha na wanaume.
Lily Joe, aliwahi kupigwa na mumewe na akaokolewa na polisi ambao walimtia mbaroni mumewe ambaye aliua wazungu wawili kwa lengo la kuwala nyama.

Hata hivyo, vyama vya kutetea haki za binadamu vinasema sheria hiyo haijajitosheleza kwa sababu bado kuna sheria zinazokandamiza wanawake kama hiyo ya mwaka 1971 inayohusisha mambo au shughuli za uchawi (practice of sorcery).

Serikali imeshaanza kuchukua hatua ya kuhakikisha unyama na ukatili wa watu kula binadamu wenzao unapigwa marufuku kwa kuanzisha mahakama za kisheria hadi vijijini na pia unahamasisha viongozi wa dini kutoa mahubiri vijijini wakiwa na ulinzi mkali ili watu waachane na unyama huo wa kuua na kula wenzao.

Pia serikali ya nchi hiyo imekuwa ikifanya juhudi kubwa ya kuwaelimisha wana vijiji na kuwafundisha ustaarabu huku ikiwajengea baadhi yao nyumba bora za kisasa na kuwapelekea nguo za kuvaa kutokana na tabia yao ya kutembea uchi wa mnyama. 

Wanawake hujifunga magome ya miti au majani maalum kuanzia kiunoni na matiti huachwa wazi ndiyo maana wanawake wengi hubakwa na kisiwa hicho kuwa hatari sana kwa wanawake kuishi.

Licha ya kufanyiwa ukatili huo, wanawake wa huko wanasifika kwa kuweza kutunza familia kwani watoto wao na waume zao licha ya kuwa na maisha duni lakini wengi wao wanakuwa na afya njema kutokana na milo wanayopewa au kuandaliwa na wanawake hao.

Wakati wanawake hujihifadhi katika sehemu hiyo ya mwili tu, wanaume wao hufunika dhakari tu kwa kutumia kibuyu maalum na sehemu nyingine zote huachwa wazi, hivyo serikali inafanya juhudi kubwa ya kuelimisha jamii hiyo hasa makabila mawili Wakuru na Wakoroi ambao ndiyo husifika kwa kula na kukausha nyama za binadamu wenzao.

Baadhi ya wanawake na wanaume wajamii hiyo.

Licha ya jitihada hizo wapo watu ambao bado wana hamu ya kula nyama za wenzao kwani wakati serikali ikifanya juhudi kufuta tabia hiyo, Wazungu wawili waliwahi kukamatwa na kuliwa nyama na polisi waliambulia kukuta vichwa tu vikiwa kwenye sufuria tayari kupikwa supu (Angalia pichani juu kulia) Wazungu hao ni kati ya wamisionari waliokuwa wakitoa huduma za kidini katika visiwa hivyo.

Habari zinasema wanaowaua wamisionari ni wanaume wa makabila hayo na hiyo ni kutokana na kuabudu mila potofu kwani hadi sasa wana maiti zilizokaushwa kwa moto katika mabanda maalum au katika mapango yaliyo jirani na vijiji vyao.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad