FIFA Ubora wa Soka Duniani: Tanzania Yapanda Nafasi 22. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, April 06, 2017

FIFA Ubora wa Soka Duniani: Tanzania Yapanda Nafasi 22.

Taifa la TANZANIA limepanda kwa nafasi 22 kwenye Viwango vya Ubora wa Soka kwa Wanaume iliyotolewa hii Leo April 06,2017 na FIFA.


Februari mwaka huu Tanzania ilikuwa nafasi ya 157 huku katika viwango vilivyotangazwa leo na FIFA ikikamata nafasi ya 135.

Timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ iliifunga Botswana mabao 2-0 kabla haijaibutua Burundi 2-1 mwishoni mwa mwezi uliopita.
Brazil imerejea kileleni kwa mara ya kwanza baada ya Miaka 6 na hili limekuja baada ya mafanikio makubwa chini ya Kocha wao Tite ambae ameshinda Mechi 9 mfululizo tangu atwae wadhifa Mwaka Jana wakifunga Bao 25 na kufungwa 2 tu.

Hivi karibuni Brazil ilishinda Mechi zake zote 2 za Kundi la Nchi za Marekani ya Kusini na kuwa Nchi ya Kwanza kufuzu kuingia Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.

Wiki iliyopita, Brazil kwanza iliifunga Uruguay 4-0 huko Montevideo na Siku 3 baadae kuichapa 3-0 Paraguay huko Sao Paolo, Brazil.

Brazil wameitoa Argentina kwenye Namba 1 ya Listi ya Ubora baada ya Argentina hivi karibuni kushinda Mechi 1 tu, walipoifunga Chile 1-0, na kisha kuchapwa 2-0 na Bolivia.

Argentina sasa wameshika Namba 2 baada kukaa kileleni kwa Miezi 12 walipowang'oa Mabingwa wa Dunia Germany ambao sasa wako Nafasi ya 3.

Katika 10 Bora Nchi pekee mpya ni Switzerland ambayo ipo wa 9 baada ya kuifunga Latvia 1-0 kwenye Mechi ya Kundi lao la Ulaya la kusaka kufuzu kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018.

Nao Vigogo Netherlands, baada ya Wiki hii kuchapwa na Bulgaria na Italy, wamezidi kuporomoka kwa Nafasi 11 na kuangukia Nafasi ya 32 ikiwa ndio Nafasi ya chini kabisa katika Historia yao.

Wengine walioporomoka mno ni Uruguay walioshuka Nafasi 6 na kuangukia Nafasi ya 15 baada Wiki hii kuchapwa na Brazil na Peru.

Wakati Egypt ndiyo Timu ya juu kabisa kwa Afrika ikishika Nafasi ya 19, Tanzania sasa ipo Nafasi ya 135 ikitokea Nafasi ya 157 baada ya kuzifunga Botswana na Burundi Nchi ambazo ziko juu yake.

FIFA LISTI YA UBORA DUNIANI – 20 BORA.

1       Brazil

2       Argentina

3       Germany

4       Chile

5       Colombia

6       France

7       Belgium

8       Portugal

9       Switzerland

10      Spain

11      Poland

12      Italy

13      Wales

14      England

15      Uruguay

16      Mexico

17      Peru

18      Croatia

19      Egypt

20      Costa Rica

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad