EPL 2016/2017- Hizi ni 6 zitakazo Ipa Ubingwa wa Ligi Kuu Chelsea au Tottenham Spurs. - Mwana Wa Makonda

Breaking

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, April 18, 2017

EPL 2016/2017- Hizi ni 6 zitakazo Ipa Ubingwa wa Ligi Kuu Chelsea au Tottenham Spurs.

Zikiwa zimebakisha mechi 6 za Ligi kuu soka Uingereza 2016/2017 kufikia tamati, kila mmoja Chelsea waliocheza mechi 32 ndio wapo kileleni wakiwa na Pointi 75 na kufuatia Tottenham Spurs wenye Pointi 71 kwa mechi pia 32.

 Wikiendi hii Chelsea na Spurs zitapambana kwenye Uwanja wa Wembley Jijini London kwenye Mechi ya Nusu Fainali ya FA CUP Mechi ambayo inasemwa itatoa morali kwa Mshindi kuelekea Ubingwa.

Kwa Mechi 6 zilizobaki kwa Timu hizi mbili, Tottenham Spurs ndio wanaonekana kuwa na Ratiba ngumu kupita Chelsea kwani wanapaswa kuzivaa Arsenal, Man United na Mabingwa Leicester City miongoni mwa Mechi zao wakati Chelsea, kimtazamo, Mechi yao ngumu ni dhidi ya Everton tu.

EPL, Ligi Kuu England 2016/2017– Mechi zilizobaki.

-U=Ugenini N=Nyumbani

Tottenham Spurs – Ratiba:

Aprili 22: Chelsea [FA Cup Nusu Fainali, Wembley]

Aprili 26: Crystal Palace [U]

Aprili 30: Arsenal [N]

Mei 6: West Ham United [U]

Mei 13 Man United [N]

Mei 18 Leicester [U]

Mei 21: Hull City [U]

Chelsea – Ratiba:

Aprili 22: Tottenham [FA Cup Nusu Fainali, Wembley]

Aprili 25: Southampton [N]

Aprili 30: Everton [U]

Mei 8: Middlesbrough [N]

Mei 12: West Brom [U]

Mei 15: Watford [N]

Mei 21 Sunderland [N]

Post Bottom Ad