Waziri wa
Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe, amesema tukio la
kutekwa kwa Roma na wenzake watatu limewashtua.
Ameda kuwa
hilo si jambo lililozoeleka Tanzania na kwamba ni lazima wafuatilie kujua kiini
chake. Akiongea na waandishi wa habari Jumatatu hii, Dkt Mwakyembe amesema
tukio hilo linaweza kuwa limefanywa na watu wachache kwaajili ya kuvuruga
mambo.
“Mimi
nawathamini sana vijana wangu hawa,” amesema Dkt Mwakyembe.
“Hawa ni
stars, hawa ndio wanainbrand Tanzania. Huyu ni bendera ya Tanzania, siwezi
kukubali tukachezeachezea watu hawa kwasababu zozote zile, ndio maana nasema
tushirikiane kwa pamoja kuhakikisha kwamba tunaviruhusu vyombo vya upepelezi
ambavyo vitafuatilia kwa ukaribu sana tupate majibu ya kile kilichotokea,”
ameongeza.
Dkt
Mwakyembe amesisitiza kuwa wizara yake ipo kwaajili ya wasanii na itawalinda
kwa namna yoyote na kwamba pale watakapoona hatari yoyote wasisite kumjulisha.
Amesema
anachosubiri ni majibu ya upepelezi ulioanza na kwamba atahakikisha anaupata na
kuusema bungeni wakati anawasilisha bajeti yake.
|
No comments:
Post a Comment