Mwanamuziki wa Tanzania, Diamond
Platnumz ameachia wimbo wake mpya kwa kushtukiza uitwao ‘Acha Nikae Kimya.’
Wimbo unazungumzia masuala mengi yanayotokea sasa ikiwemo hofu iliyotanda baada
ya Msanii Roma Mkatoliki na wenzie kutekwa.
Wimbo huo
hata hivyo umepokelewa kwa hisia tofauti.
Hizi ni
sababu zake kwanini ameamua kuuachia:
Ili Nchi
ipate maendeleo inahitaji Upendo na Ushirikiano wa Wananchi na Serikali..Na
Nikiwa kama Msanii, jukumu langu ni kuhakikisha natumia Hekma na busara kukemea
jambo nilionalo haliko sawa ili lirekebishwe, lakini pia panapokuwa hakuna
maelewano jukumu langu pia ni kupatanisha ili kwa pamoja tujenge nchi yetu
kusudi wazazi wetu, watoto pamoja na familia zetu waishi kwa Upendo Amani na
kufurahia nchi yetu…Na ndiomaana kwenye nyimbo nakwambia “MI NA WEWE WA TAIFA
MOJA…KAMBARAGE BABA MMOJA….SASA TOFAUTI ZA NINI TUSHIKAMANE TUKAIJENGE
TANZANIA”…
Unatakiwa
utambue kuwa kila kiongozi ni Binadamu na kama wote tujuavyo, Binadamu
hatujakamilika… hivyo katika nchi yoyote lazma wakati mwingine kuna jambo
linaweza likawa haliko sawa, ila sisi kama wananchi tunatakiwa tutumie Hekima
na Busara kwenye kufikisha ujumbe ama hoja zetu ili viongozi walieke
sawa…Busara na Hekima itafanya viongozi watuelewe kirahisi na pengine mengi
tuyatakayo tutimiziwe kirahisi… mfano mzuri, juzijuzi kupitia kipindi cha
Clouds360 cha clouds Tv nlipopata bahati ya kuongea na Mh Raisi nilimuomba
atufungulie Mabanda ya Chipsi na Bodaboda ziruhusiwe kufanyakazi hadi asubuhi
maana zilikuwa nwisho saa 4 ama 5 usiku…kwakuwa nilitumia Hekima na busara
kwenye Kufikisha hoja ama Ombi langu..alikubali na tukapewa ruksa na sasa hivi
maeneo mengi ya Chipsi na Bodaboda yanafanya kazi hadi usiku mnene…
.....hivyo
tusikubali tu kulishwa Sumu za kuleta ugomvi kati yetu wenyewe kwa wenyewe eti
Mara Tutukane mara sijui fanyeni hiki, wakati hata baadhi ya wanaochochea mambo
hayo hawaishi Tanzania wanaishi Ulaya / Marekani / kifupi nje ya nchi…ikija
kutokea bahati mbaya kimenuka wao watakuwa wanakula kuku kwa mrija huko
walipo.
…halafu sisi na familia zetu ndio tutateseka na kuhaha kunusuru roho zetu
usiku kucha.. Hatutaki makelele ya Uchonganishi mitandaoni, kama mtu kweli
anauchungu na nchi na kweli akisemacho anamaanisha aje, na kwa pamoja twende
sehemu husika kupeleka malalamiko sio kukaa kitandani kupost kuchochea Ugomvi
kumbe anatuchora na kutufanya kama sie mataahira wake, anatupeleka mara kushoto
mara kulia… Akikaa pekeake anatucheka kuwa sie wajinga wake katueka mkononi…
|
No comments:
Post a Comment