Mbunge wa
Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nasari na Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe jana walichafua hali ya hewa bungeni na
kusababisha mzozo mkubwa katika mjadala uliokuwa ukiendelea.
Wawili hao
walihamisha mjadala wa hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais Tamisemi na kurudisha
suala la Richmond lililotokea mwaka 2008, huku Nasari akimtuhumu Dk Mwakyembe
kuwa hakutenda haki katika ripoti yake na kumuondoa bila kumpa nafasi ya
kujitetea aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.
“Huyu
Mwakyembe ndiye aliyeongoza ripoti ya Richmond na hakumpa nafasi mheshimiwa
Lowasa ajitetee, leo tena kapewa dhamana ya kuongoza Wizara ya Habari, Nape
(Nnauye) ameondolewa lakini hakuna nafasi ya kumhoji Mkuu wa Mkoa... hakuna
haki hapo,” alisema.
Kauli za
Nasari zilimfanya Dk Mwakyembe kuomba mwongozo na aliposimama alisema:
“Nilikuwa naongoza kamati na utaratibu mzuri wa kisheria ni kuwa, kama utaona
kuna ushahidi wa kutosha hakuna sababu ya kumuita mtu, unaleta taarifa bungeni
halafu Bunge linakuja kuamua.”
Dk Mwakyembe
alisema katika taarifa yao, waliona hakuna sababu ya kumuita Lowassa kuhojiwa
kwani ushahidi ulikuwa wazi na ndiyo maana hakutakiwa kuitwa mbele ya kamati
badala yake walikuja kumshtaki bungeni.
“Huyu mtu
wanayekuwa na mahaba naye kwa sasa, nasema wamlete hata leo waone kama
hatutamnyoa kwa chupa, kanuni za kibunge zinaruhusu anaweza kuirudisha tena
taarifa ya Richmond na ikaanza upya,” alisema Dk Mwakyembe.
|
No comments:
Post a Comment