VPL 2016/2017:Yanga SC Yajipoza kwa Ruvu Shooting. - Mwana Wa Makonda

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, March 01, 2017

VPL 2016/2017:Yanga SC Yajipoza kwa Ruvu Shooting.


Baada ya Yanga SC ya Dar es Salaam kupoteza mchezo kwa kufungwa goli 2-1 dhidi ya watani zao wa jadi Simba SC siku ya Jumamosi ya February 25,2017, leo Jumatano ya March 01, 2017 ilicheza mchezo wake wa kiporo dhidi ya Ruvu Shooting uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mabingwa hao watetezi wa taji la ligi kuu Tanzania bara, Yanga SC, wameibukia kwa Ruvu Shooting na kuitandika magoli 2-0 kwenye mechi hiyo kwa  goli  la mkwaju wa penati baada ya beki wa Ruvu Shooting kuushika mpira akiwa kwenye eneo la box , Mpigaji wa penati wa Yanga SC, Simon Msuva.

Wakati mechi inaelekea ukingoni, Emanuel Martin aliyeingia akitokea benchi, aliifungia Yanga SC bao la pili na la ushindi  kwa kichwa alipounganisha pasi ya Musuva na kumwacha golikipa wa Ruvu Shooting , Bidii Hussein akiwa hoi baada ya kujaribu kuufata mpira na kujigonga kwenye nguzo ya goli.

Ushindi huo sasa unaifanya Yanga SC kuendelea kuwa na nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu msimu huu 2016/2017 kwa kufikisha jumla ya point 52 nyuma ya watani zao Simba SC  wanaoongoza Ligi kwa kuwa na jumla ya point 54, Ruvu wao bado wapo nafasi ya 10 kwa kuwa na point 28 wakicheza mechi 24, Yanga SC sasa atacheza dhidi ya Mtibwa Sugar siku ya Jumapili March 05, 2017,katika uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Ligi hiyo ambayo ni michuano mikubwa nchini, itaendelea mwishoni mwa wiki hii ambako kwa siku ya Jumamosi Machi 04, mwaka huu 2017, Simba SC itacheza na Mbeya City kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ukiacha mchezo huo, michezo mingine ya Jumamosi Machi 04, mwaka huu itakuwa ni kati ya Toto Africans na Mbao FC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza huku Kagera Sugar ikiikaribisha Majimaji FC ya Songea kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Azam FC pia itacheza Jumamosi Machi 04, mwaka huu na Stand United ya Shinyanga kwenye Uwanja wa Chamazi. Mchezo huo utaanza saa 1.00 jioni wakati mechi nyingine zitaanza saa 10.00 jioni.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limerejesha tena mechi za Ligi Kuu kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro na Jumapili Machi 05, mwaka huu Mtibwa Sugar itaialika Young Africans kwenye uwanja huo katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Mchezo mwingine wa Ligi Kuu ya Vodacom utachezwa Uwanja wa Uhuru ambako African Lyon itaialika Mwadui FC ya Shinyanga wakati Ndanda FC itakuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Post Bottom Ad