Ujumbe wa Waziri Mwigulu Mtandaoni:...Nape Sio Jambazi…'' - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, March 24, 2017

Ujumbe wa Waziri Mwigulu Mtandaoni:...Nape Sio Jambazi…''

Waziri Nchemba akiwa na Nape Moses Nnauye.

Waziri wa mambo ya ndani nchini Tanzania,Mhe. Mwigulu Nchemba ameshutumu kitendo cha askari mmoja kuchomoa bastola na kufyatua risasi wakati maafisa wa usalama walipokuwa wanajaribu kumzuia aliyekuwa waziri wa habari kuhutubia wanahabari.

Mhe.Nchemba, kwenye ukurasa wake wa Facebook, amesema kitendo hicho si cha busara na kwamba afisa mhusika kuadhibiwa.
Amesema amemwagiza mkuu wa jeshi la polisi kutumia picha zilizopigwa wakati wa tukio hilo kumsaka mhusika.

"Nape Moses Nnauye sio jambazi, ni Mtanzania, ni mbunge, mjumbe wa NEC wa CCM, hana rekodi ya uhalifu. Kitendo cha mtu kumtolea bastola, sio cha kiasikari, sio cha Kitanzania na sio cha ki Mungu, kama mtu ameweza kutoa bastola mbele ya kamera nawaza mbali ingekuwa kwenye uchochoro angefanya nini," ameandika.

"Nahusika na usalama wa raia wote wa Tanzania, nimemwelekeza IGP atumie picha kumsaka mtu yule aliyeinua kufanya kitu cha kihalifu kwa kofia ya uaskari. Na kama ni askari basi sheria zinazoongoza taasisi husika zichukue mkondo wake.

Katika hatua nyingine, Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amewashukuru waandishi wa habari kwa mchango wao pamoja na upendo waliomuonyesha wakati wa uwaziri wake.

Mbunge huyo wa jimbo la Mtama, amesema hayo kupitia Twitter:

..Wanahabari mme GUSA sana moyo wangu!Sikujua kama mnanipenda na kunithamini kiasi KILE!Nawashukuru SANA kwa kujitolea kwenu!Nawapenda SANA!

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad