Taswira Picha:RC Makonda aanza kuhojiwa na Bunge -Dodoma. - Mwana Wa Makonda

Breaking

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, March 29, 2017

Taswira Picha:RC Makonda aanza kuhojiwa na Bunge -Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda leo,March 29,2017 amefika mbele ya kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kufuatia wito wa Kamati hiyo kumtaka afike mbele ya kamati kujibu tuhuma zinazomkabili za kuingilia Haki, Uhuru na Madaraka ya Bunge kutokana na matashi aliyoyatoa mapema mwezi februari 2017 jijini Dar es Salaam yaliyokuwa na madai ya kudharau Bunge.
Wito wa kufika mbele ya Kamati hiyo unafuatia Azimio la Bunge lilitolewa tarehe 8 Februari 2017 ambapo Bunge liliazimia Mhe. Spika aweze kukubali Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Alexandra Mnyeti na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda wahojiwe kutokana na Matamshi yao ya Kudharau Bunge.Post Bottom Ad