Taswira Picha Gari dogo aina ya Toyota Carrina lapata Ajali Rulenge na kuua Mchezaji wa Benaco FC. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, March 06, 2017

Taswira Picha Gari dogo aina ya Toyota Carrina lapata Ajali Rulenge na kuua Mchezaji wa Benaco FC.

Mtu mmoja amefariki dunia na Watu wawili  wamejeruhiwa na wamelazwa katika hospitali ya Nyamiaga wilayani Ngara,mkoani Kagera baada ya kutokea ajali iliyohusisha gari dogo aina ya Toyota Carrina  yenye namba za usajili T 619 CFP, katika eneo la Nyamahwa tarafa ya Rulenge.

Aliyefariki ni Mchezaji wa Timu ya Benaco FC Nuru Athuman akiwa na wenzake kwenye gari dogo hilo wakielekea Rulenge kucheza mechi ya kirafiki na Timu ya Rulenge Stras.


Waliojeruhiwa ni Kaimu Katibu mkuu wa Chama cha Soka wilaya ya Ngara-NDFA, Jophram na Nahodha wa Benaco FC Mpoto Mpoto ambao wamelazwa hospitali ya Nyamiaga kwa matibabu zaidi.

Mashuhuda wa ajali hiyo wanaeleza kuwa  chanzo cha ajali hiyo huenda imesababishwa na Mwendo kasi na kusababisha gari kutoka pembeni mwa barabara.

Mtandao huu unatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na familia ya mpira Wilayani Ngara, Kagera.

Post Bottom Ad