Tanzania Rwanda na Burundi zimeorodheshwa kuwa kati ya nchi zenye watu wasio na Furaha Duniani. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, March 21, 2017

Tanzania Rwanda na Burundi zimeorodheshwa kuwa kati ya nchi zenye watu wasio na Furaha Duniani.

Tanzania Rwanda na Burundi zimeorodheshwa kuwa kati ya nchi zenye watu wasio na furaha duniani.

Rwanda iko nafasi ya 151 , Tanzania nafasi ya 153 huku Burundi ikiwa nafasi ya 154 kati ya nchi 155.

 Norway ndiyo imechukua nafasi ya kwanza kama nchi yenye watu walio na furaha zaidi duniani, kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa na kumshinda jirani wake Denmark, ambayo ichukua nafasi ya kwanza mwaka uliopita.

Mwanamke mwenye huzuni
Ripoti hiyo inaangazia furaha watu waliyo nayona ni kwa nini.

Denmark, Iceland, Uswisi na Finland zinachukua nafasi tatu za kwanza huku nchi ya Jamhuri ya Afrika ya katika ikichukua nafasi ya mwisho kati nchi zenye watu wasio na faraha duniani.

Mataifa ya magharibi mwa Ulaya na Marekani pia nayo yako na watu wenye furaha duniani wakati Marekani ikichukua nafasi ya 14 na Uingereza nafasi ya 19.

Nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara na zile zinazokumbwa na mizozo, zina alama za chini.

Syria ilichukua nafasi ya 152 kati ya nchi 155 huku Yemen na Sudan Kusini, nchi zinazokumbwa na njaa zikichukua nafasi za 146 na 147 mtawalia...

Na:BBC Swahili.


Haki miliki ya picha

Nchi zenye watu walio na furaha na wasio na furaha Duniani
Nchi zenye watu walio na furaha DunianiNchi zenye watu wasio na furaha Duniani
1. Norway146. Yemen
2. Denmark147. Sudan Kusini
3. Iceland148. Liberia
4. Uswizi149. Guinea
5. Finland150. Togo
6. Uholanzi151. Rwanda
7. Canada152. Syria
8. New Zealand153. Tanzania
9. Australia154. Burundi
10. Sweden155. Jamhuri ya Afrika ya Kati

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad