Serengeti Boys na Kambi ya Wiki moja mkoani Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, March 28, 2017

Serengeti Boys na Kambi ya Wiki moja mkoani Kagera.

Timu ya taifa ya mpira wa miguu ya vijana wenye umri wa miaka 17, Serengeti Boys imeondoka kwenda mkoani Kagera wameenda na ndege ya (ATCL) kutoka Dar es Salaam, alfajiri ya Machi 26, mwaka huu kwa kambi ya wiki moja.

Serengeti Boys itakuwa kambini Bukoba hadi Aprili 02, mwaka huu,2017 ambako inatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya timu vijana ya Burundi kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba mkoani Kagera. Michezo hiyo itafanyika Machi 30, 2017 na kurudiana Aprili mosi, mwaka huu.

 Serengeti Boys ambayo inajiandaa na michuano Afrika huko Gabon itarejea Dar es Salaam Aprili 2, mwaka huu ambako imepangwa kucheza na Ghana Aprili 3, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mchezo huo utatanguliwa na hafla ya kuagwa kwa kukabidhiwa bendera.

Timu itaelekea Morocco Mei 5, mwaka huu baadaye itapita Cameroon kwenye kambi ya zaidi ya mwezi mmoja baadaye itakwenda Gabon katika michuano itakayoanza Mei 14, 2017. Ikiwa Cameroon itacheza mechi mbili za kimataifa dhidi ya wenyeji kabla ya kwenda kwenye fainali.

Serengeti Boys ni timu ya vijana ambayo imefuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika Gabon kuanzia Mei 14, mwaka huu. Timu hiyo imepangwa Kundi ‘B’ pamoja na mabingwa watetezi Mali, Niger na Angola. Ina lengo la kurejea na Kombe la Afrika kwa vijana.

La ikitokea imekosa nafasi hiyo angalau ikafika nusu fainali ambako kwa mafanikio hayo itakuwa tayari ina tiketi mkononi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia huko India, Novemba, mwaka huu,2017.

Kikosi cha Serengeti Boys kinaundwa na Makipa:-

 Ramadhan Kabwili

 Samwel Edward 

na Kelvin Kayego.

Walinzi:-

 Kibwana Ally Shomari

 Nickson Kibabage

 Israel Mwenda

 Dickson Job

 Ally Msengi

 Issa Makamba 

na Enrick Vitalis Nkosi.

Viungo:-

 Kelvin Nashon Naftali

 Ally Ng’anzi

 Mohamed Rashid

 Shaaban Ada

 Mathias Juan

 Marco Gerald

 Abdulhamis Suleiman

 Saidi Mussa 

na Cyprian Benedictor Mtesigwa.

Washambuliaji:-

 Muhsin Malima Makame

Yohana Mkomola

 Ibrahim Abdallah

 Assad Juma 

na Abdul Suleiman.

Benchi la Ufundi:-

Bakari Shime (Kocha Mkuu)

Oscar Mirambo (Kocha Msaidizi)

Muharami Mohamed (Kocha wa makipa)

Kim Poulsen (Mshauri wa Ufundi)

Edward Evans (Mtunza Vifaa)

Shecky Mngazija (Daktari wa timu)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad