Ratiba ya robo Fainali ya UEFA Champios League na UEFA Europa League 2016/2017 - Mwana Wa Makonda

Breaking

X-BET


Post Top Ad

Friday, March 17, 2017

Ratiba ya robo Fainali ya UEFA Champios League na UEFA Europa League 2016/2017

Ratiba ya robo fainali ya UEFA Europa League 2016/2017.

DROO ya kupanga Mechi za Robo Fainali za UEFA Champions League imefanyika Mchana wa leo March 17,2017 huko Nyon, Uswisi kwenye Makao Makuu ya UEFA na Mabingwa Watetezi Real Madrid kupangwa na Bayern Munich.

Mabingwa wa England Leicester City wao wamepangwa kucheza na Atletico Madrid wakati Barcelona wakicheza na Juventus na Borussia Dortmund kuivaa AS Monaco. 

ROBO FAINALI – DROO KAMILI.

-Atletico Madrid v Leicester City

-Borussia Dortmund v AS Monaco

-Bayern Munich v Real Madrid

-Juventus v Barcelona

Mechi za Robo Fainali zitachezwa Aprili 11 na 12 na Marudiano ni Aprili 18 na 19.

Nayo  DROO ya Mechi za Robo Fainali ya UEFA EUROPA LIGI imefanyika Leo huko Nyon, Uswisi kwenye Makao Makuu ya UEFA na Manchester United kupangwa kucheza na Anderlecht ya Belgium.

Timu anayochezea Staa mkubwa wa Tanzania, Mbwana Samatta, KRC Genk ya Belgium, wao watawavaa Celta Vigo ya Spain.

Mechi nyingine ni kati ya Ajax na Schalke wakati Lyon ya France wakicheza na Besiktas ya Uturuki.

Robo Fainali – Droo kamili.

-Anderlecht v Manchester United

-Celta Vigo v KRC Genk

-Ajax v Schalke

-Lyon v Besiktas

Mechi za Robo Fainali zitachezwa Aprili 13 na Marudio ni Aprili 20.

Post Bottom Ad