Ramadhan Singano ‘Messi’ Aipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Mbabane Swallows. - Mwana Wa Makonda

Breaking

X-BET


Post Top Ad

Monday, March 13, 2017

Ramadhan Singano ‘Messi’ Aipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Mbabane Swallows.

Ramadhani Singano 'Messi' akimtoka beki wa Mbabane Swallows, Sifio Mabila.

Goli la dakika ya 84 ya mchezo la mchezaji Ramadhan Singano ‘Messi’ limewapa Azam FC ushindi finyu wa 1-0 dhidi ya Mbabane Swallows ya Swaziland kwenye Mechi ya Kwanza ya raundi ya Kwanza ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho iliyochezwa huko Azam Complex, Chamazi, kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam.
Salum Abubakar 'Sure Boy' akimiliki mpira mbele ya kiungo wa Mbabane, Kabamba Tshishimbi.

Timu hizi zitarudiana huko Mbabane, Swaziland Wikiendi ijayo na Mshindi kusonga Raundi ya Mchujo na kupambanishwa na moja ya Timu 16 zitakazotolewa kwenye Raundi ya Kwanza ya CAF Champions League.

Washindi wa Raundi ya Mchujo watasonga Hatua ya Makundi ya CAF Kombe la Shirikisho ambako kutakuwa na Makundi Manne ya Timu 4 kila moja.

Post Bottom Ad