Picha Uzinduzi wa Tawi la Simba SC ''Kichwabuta'' mjini Bukoba-Kagera. - Mwana Wa Makonda

Breaking

X-BET


Post Top Ad

Thursday, March 30, 2017

Picha Uzinduzi wa Tawi la Simba SC ''Kichwabuta'' mjini Bukoba-Kagera.

Kushoto ni Makamu Rais wa Klabu ya Simba SC, Geofrey Nyange Kaburu katika picha ya Furaha na Wanachama wa Simba SC wakati wa uzinduzi wa Tawi Jipya  la Wanachama wa Klabu hiyo Mjini Bukoba mkoani Kagera,March 29,2017 likiwa na  Wanachama zaidi ya 220  na kupewa jina la KICHWABUTA.


Tawi hilo linawanachama 60 walio hai na wanaosubiri kukabidhiwa Kadi za Uanachama na Uongozi wa Klabu ya Simba SC huku wengine 160  wakiwa tayari nao wamekamilisha taratibu za kuwa wanachama hai.
Mwenyekiti wa Muda wa Tawi hilo Prisius Massai maarufu kwa jina la Majeshi amesema uzinduzi wa tawi hilo umeenda sambamba na ufunguzi wa Ofisi katika eneo la Hamgembe mjini Bukoba ikiwa ni hatua yao ya kuiunga mkono Klabu ya Simba SC yenye makao makuu yake Jijini Dar Es Salaam.

Massai anasema pamoja na kuhamasisha wapenzi wa Simba SC mkoani Kagera kujiunga katika Tawi lao ili kukuza mahusiano na wanatarajia umoja huo uwanufaishe kwa kupanua wigo kwa kutoka kwenye ulipaji wa ada ya mwaka na kufungua mfuko wa Tawi au SACCOS  ili kuwasaidia wanachama kuleteana uchumi na maendeleo.
 
Tawi hilo la Wanachama wa Simba SC Manispaa ya Bukoba mkoani Kigoma limepewa Jina la KICHWABUTA ikiwa ni kuenzi Kazi kwa Vitendo ya Marehemu Mzee Omary Hussein Kichwabuta ambaye alikua ni Mwanachama na Shabiki mkubwa wa Simba SC.


Post Bottom Ad