Leicester City -Timu Pekee toka Ligi ya EPL kufuzu Robo fainali UEFA Champions League 2016/2017. - Mwana Wa Makonda

Breaking

Post Top Ad

Thursday, March 16, 2017

Leicester City -Timu Pekee toka Ligi ya EPL kufuzu Robo fainali UEFA Champions League 2016/2017.

Matokeo ya mechi za UEFA Champions League zilizochezwa usiku wa March 15 2017, Atletico Madrid na AS Monaco wanafuzu kucheza robo fainali.

Jumatano 15, Machi 2017.

Atl├ętico Madrid 0 Bayer 04 Leverkusen 0 [4-2]   
           
Monaco 3 Manchester City 1 [6-6, Monaco yasonga kwa Bao za Ugenini]  
 
Baada ya michezo ya Jana March 15,2017 usiku , timu nane zimefanikiwa kuingia hatua ya robo fainali klabu bingwa ulaya Au UEFA Champions League msimu wa 2016/2017.

ROBO FAINALI – WALIOFUZU

-Real Madrid [Mabingwa Watetezi]

-FC Barcelona

-Bayern Munich

-Borussia Dortmund

-Juventus

-Leicester City

-Atletico Madrid

-AS Monaco
Droo ya Mechi za Robo Fainali itafanyika Kesho Ijumaa March 17,2017 na Mechi zake kuanza kuchezwa Aprili 11 na 12,2017.

Katika timu zilizofuzu, Leicester City pekee ndio timu iliyofanikiwa kusonga mbele katika michuano hiyo ikitoka katika ligi maarufu zaidi duniani ya England.

 Hii ni tofauti kwa ligi ya Hispania ' La liga ' waliotoa timu tatu ; FC Barcelona, Atletico Madrid na Real Madrid.

Post Bottom Ad