Kenya yasoma Bajeti yake ya Mwaka 2017 na 2018. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, March 31, 2017

Kenya yasoma Bajeti yake ya Mwaka 2017 na 2018.

Nchi ya Kenya imesoma Bajeti yake ya mwaka 2017/2018, hapo Jana March 30,2017 kinyume na inavyosomwa kawaida mwezi Juni, kutokana na Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Agosti mwaka huu 2017, huku ikitangaza kusimamisha ajira katika sekta ya umma.

Katika Bajeti hiyo ya shilingi za Kenya Trilioni 2.6 (Takriban shilingi trilioni 52 za Tanzania) ambapo Waziri wa Fedha wa nchi hiyo, Mhe.Henry Rotich ameondoa kodi kwenye mahindi yanayoagizwa kutoka nje kwa kipindi cha miezi minne ijayo,

Aidha kodi imeondolewa kwenye dawa za kuulia wadudu za nchini humo pamoja na magari ya utalii yanayoundwa nchini Kenya.

Katika bajeti hiyo ambayo ni ya mwisho kwa serikali ya Jubilee katika muhula wake wa kwanza, serikali imeongeza kodi kwenye kamari hadi 50% kutoka 7.5% ya awali kama njia ya kukomesha uchezaji kamari.

Serikali pia imetangaza kusimamisha ajira katika sekta za umma isipokuwa sekta ya elimu kama njia ya kupunguza matumizi.

Jumla ya Shilingi bilioni 524.6 za kenya katika Bajeti hiyo zitatokana na mikopo kutoka nje na ndani ya nchi.

Shilingi bilioni 2 za Kenya  zimetengwa kuwaajiri walimu, na zingine bilioni 4 kuwalipia mtihani wanafunzi wa darasa la nane na kidato cha nnemwaka 2017 na 2018 huku serikali za kaunti zikipata jumla la shilingi bilioni 329.

Ili kuhakikisha kuwa vijana wana ajira, serikali imetenga shilingi milioni 450 Ksh kwa kuboresha kiwanda cha Rivatex, na zingine milioni 250 kuboresha kiwanda cha Maziwa cha New KCC.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad