Kandarasi ya Miaka 2 ya Kocha HANS VAN DER PLUIJIM Singida United. - Mwana Wa Makonda

Breaking

X-BET


Post Top Ad

Saturday, March 18, 2017

Kandarasi ya Miaka 2 ya Kocha HANS VAN DER PLUIJIM Singida United.

Aaliekuwa kocha wa Yanga SC, Mholanzi Hans Van der Pluijm amejiunga na klabu ya Singinda United iliyopanda Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu ujao wa 2017/2018.


Na Pluijm anaamua kwenda Singida United baada ya kusitishiwa mkataba wa Ukurugenzi wa Ufundi wa Yanga wiki iliyopita.

Yanga SC ilimhamishia Pluijm kwenye Ukurugenzi wa Ufundi Novemba mwaka jana,2016 baada ya kumleta Mzambia, George Lwandamina awe kocha Mkuu.
Pluijm amefundisha Yanga SC kwa awamu mbili tangu mwaka 2014 alipoanza kwa kufanya kazi kwa nusu msimu, akimpokea Mholanzi mwenzake, Ernie Brandts kabla ya kwenda Uarabuni.

Singida United imerejea Ligi Kuu msimu huu baada ya msoto wa zaidi ya miaka 15 tangu ishuke Daraja.  Post Bottom Ad