Kambi za wakimbizi mkoani Kigoma Zaelemewa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, March 18, 2017

Kambi za wakimbizi mkoani Kigoma Zaelemewa.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga na Mwakilishi wa Shirika linalohudumia wakimbizi nchini (UNHCR), Chansa Kapaya kwa pamoja wakikabidhi zawadi kwa baadhi ya watoto wakimbizi waliofanya vizuri kwenye masomo yao wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani 2016 yaliyobeba kauli mbiu “Tupo Pamoja na wakimbizi. Tafadhali ungana nasi.”  ambapo kitaifa yamefanyika katika kambi ya Nyarugusu, wilayani Kasulu, mkoani Kigoma…Picha na Maktaba yetu.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga amesema idadi ya wakimbizi waliopo mkoani humo ni ni kubwa, tofauti na uwezo wa kambi zilizopo.

Maganga amesema hayo wakati akizungumzia uamuzi wa kuanza kuwadhibiti wakimbizi wanaoingia Kigoma kutoka nchi za DRC, Burundi na Rwanda wanaoingia kila siku hapa nchini.

Mkuu huyo wa mkoa amesema kambi zilizopo Kigoma zinaweza kuhifadhi watu 150,000, lakini waliopo sasa ni zaidi ya 300,000.

Tayari mkoa huo umesema kuwa wastani wa kati ya Wakimbizi 500 hadi 520 kutoka DRC na Burundi huingia mkoani Kigoma kila siku kwa ajili ya kuomba hifadhi.

Mkoa wa Kigoma una kambi tatu za wakimbizi ambazo ni Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu, Nduta iliyopo Kibondo na Mtendeli katika Wilaya ya Kakonko.

 “Tumeunda kamati ya kuwahoji kabla ya kukubaliwa kupata hifadhi ya ukimbizi,” amesema.

Post Bottom Ad