Hii ndio Orodha ya Wagombea Ubunge Africa Mashariki waliopitishwa kupitia CCM. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, March 29, 2017

Hii ndio Orodha ya Wagombea Ubunge Africa Mashariki waliopitishwa kupitia CCM.

Chama cha Mapinduzi (CCM) Nchini Tanzania, kimetangaza majina ya Wanachama wake 12 walioteuliwa kugombea Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Uchaguzi unaotarajiwa kufanyika kwenye mkutano wa Bunge ujao.

 Akisoma majina hayo leo,March 29,2017 wakati wa Mkutano na waandishi wa habari, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema kuwa wameteua wananchama hao miongoni mwa wengi zaidi ya 400 waliokuwa wamechukua fomu kugombea nafasi hizo.

Mchanganuo.

Miongoni mwa Wabunge 9 watakaokwenda Bunge la Afrika Mashariki kuiwakilisha Tanzania, 6 watatoka CCM. 

Kufuatia idadi, hiyo CCM imesema kuwa itatoa wabunge watatu wa kiume na watatu wa kike ambapo miongoni mwao wanne watatokea Tanzania Bara na wawili watatokea Tanzania Visiwani.

Walioteuliwa kugombea nafasi hizo ni;

Wanawake Tanzania Bara;

        Zainabu Rashid Mafaume Kawawa

        Happiness Elias Lugiko

        Fancy Haji Nkuhi

        Happiness Ngoti Mgalula

Wanaume Tanzania Bara;

        Dkt Ngwaru Jumanne Maghembe

        Adam Omari Kimbisa

        Anamringi Issay Macha

        Charles Makongoro Nyerere

Wanawake Zanzibar;

        Maryam Ussi Yahya

        Rabia Abdallah Hamid

Wanaume Zanzibar;

        Abdallah Hasnu Makame

        Mohammed Yussuf Nuh

Miongoni wa wagombea hawa 12, Bunge litapiga kura kuchagua wabunge sita watakaoiwakilisha Tanzania kwenye Bunge la Afrika Mashariki kwa tiketi ya CCM.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad