DC:Ashangazwa na Ujasiri wa Wakulima wa Bangi. - Mwana Wa Makonda

Breaking

X-BET


Post Top Ad

Friday, March 31, 2017

DC:Ashangazwa na Ujasiri wa Wakulima wa Bangi.

Mkuu wa Wilaya ya Nzega, mkoani Tabora, Bw.Godfrey Ngupula ameshangazwa na ujasiri walionao wananchi wanaolima mashamba makubwa ya bangi kwa kujiamini kama hakuna serikali.

Akizungumza na Wanahabari wakati akiwa kwenye operesheni ya kukamata na kuteketeza bangi,alisema baadhi ya wananchi wamegeuza hifadhi ya Igombe iliyopo mpakani mwa wilaya za Nzega kugeuzwa kuwa mashamba ya bangi.

 “Sijawahi kuona watu wanalima bangi kwa kujiamini kiasi hiki tena kwa wingi kama hakuna Serikali, tutahakikisha bangi yote inateketezwa na watuhumiwa wote kufikishwa mahakamani,” alisema Ngupula.

Aidha Mkuu wa Polisi Wilaya ya Nzega, Costantine Mbogambi alisema jeshi hilo litapiga kambi msituni kuhakikisha mashamba yote yanateketezwa.

Na Emmy Mwaipopo

Post Bottom Ad