CCM MPYA: Yamfukuza Uanachama Sophia Simba na Ramadhani Madabida. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, March 12, 2017

CCM MPYA: Yamfukuza Uanachama Sophia Simba na Ramadhani Madabida.

Bi.Sophia Simba.

Chama cha Mapinduzi katika mkutano wake mkuu unaoendelea Dodoma, Nchini Tanzania, Jumamosi ya March 11, 2017,kimemfukuza mwanachama wake mkongwe na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Bi.Sophia Simba.

Wakati huo huo chama kimetoa msamaha kwa Adam Kimbisa na kimempa onyo kali Emmanuel Nchimbi wote ni wanachama wa CCM. 

Imeelezwa kuwa onyo kali alilopewa Nchimbi lina maana ya kuwa hatoruhusiwa kugombea nafasi yoyote kwa kipindi cha miaka minne.

Katika taarifa hizo za Chama, Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida amefukuzwa pia.

Aidha  baadhi ya wananchama wa CCM wamevuliwa uanachama huku wengine wakipewa onyo kali kwa sababu mbalimbali, kubwa ikiwa ni usaliti katika uchaguzi mkuu mwaka 2015.

Kufuatia maamuzi hayo, Sophia Simba amepoteza rasmi nafasi yake ya Ubunge wa Viti maalumu na Uenyekiti wa UWT kwani nafasi hizo zinahitaji mtu ambaye ni mwanachama wa chama aweze kuzishika.

Kwa hivyo, CCM italazimika kupeleka jina jingine Tume ya Uchaguzi kuteua mbunge wa kuziba nafasi ya Sophia, huku nafasi yake ya Uenyekiti UWT ikisubiri uchaguzi baadae mwaka huu.

SOMA HAPA CHINI TAARIFA RASMI.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad